Rais Ufaransa kuwasilisha mswada usaidizi wa kufa

RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron anakusudia kupendekeza mswada wa kuhalalisha msaada wa kufa kwa wagonjwa mahututi.

Katika mahojiano yaliyochapishwa leo Jumatatu kwenye gazeti la Liberation la Ufaransa, Macron amesema anapanga kuwasilisha mswada huo bungeni mwezi Mei.

Taarifa ya mtandao wa Al-Jazeera ambao umenukuu kutoka katika chanzo hicho, imeeleza mswada huo utawahusu watu wazima wanaougua magonjwa ya muda mfupi hadi ya kati.

Magonjwa hayo ni pamoja na saratani ya hatua ya mwisho. Hatua hiyo inakuja huku nyuma kukiwa na uungwaji mkono na baadhi ya wananchi.

Sheria hiyo, Macron aliliambia gazeti la Ufaransa Liberation, “inafuatilia njia ambayo haikuwepo hadi sasa na ambayo inafungua uwezekano wa kuomba msaada wa kufa chini ya masharti fulani magumu”.

Macron ameongeza kuwa mswada huo utawaruhusu watu wazima wanaougua ugonjwa usiotibika na wenye uwezo wa kutoa maoni yao wenyewe kuagizwa dawa ya kuua ambayo wagonjwa watajisimamia wenyewe au kwa usaidizi wa mtu mwingine

Habari Zifananazo

Back to top button