Rais wa Madagascar avunja serikali

MADAGASCAR : RAIS wa Madagascar, Andry Rajoelina, ameivunja serikali yake jana Jumatatu baada ya machafuko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu 22, kulingana na taarifa zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.
Rajoelina alitangaza hatua hiyo kupitia hotuba ya taifa kwa njia ya televisheni, akisema ameamua kusitisha shughuli za Waziri Mkuu Christian Ntsay na mawaziri wengine. Hata hivyo, wawakilishi wa serikali watabaki madarakani kwa muda hadi serikali mpya itakapoundwa.
Rais pia ametoa siku tatu za kupendekeza Waziri Mkuu mpya, akiwahakikishia raia kuwa ameyasikia madai yao na kuomba radhi kwa niaba ya watumishi wa serikali wazembe. SOMA: MSD yaitembelea taasisi mwenza ya Madagascar