PICHA| RC ashinda kesi ya ulawiti

ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda, amesema anashukuru hukumu ya mahakama kutokana na kesi ya kudaiwa kulawiti iliyokuwa inamkabili na kusisitiza kuwa haki imetendeka na mambo mengine yaliyotokea anamuachia Mungu.

Dk. Nawanda ameshinda Kesi ya Jinai namba 18853/2024.iliyokuwa inamkabili katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Mwanza.

Alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 9 na kusomewa shtaka moja la kulawiti kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.

Advertisement

Akisoma hukumu hiyo leo , Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Erick Marley, amesema kuwa jumla ya mashahidi 10 kati ya 11 waliowasilishwa na upande wa Mashitaka walitoa ushahidi wao mahakamani na kwamba ushahidi huo umeshindwa kumtia hatiani mshitakiwa, hivyo mahakama imemwachia huru.

Dk. Nawanda alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 9 na kusomewa shtaka moja la kulawiti kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.