RC Kigoma ahamamisha wananchi uchaguzi mitaa

MKUU wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye amewata wananchi wa mkoa huo kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wakaazi kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa.
RC Andengenye amesema vitambulisho vya kupigia kura vilivyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) havitatumika kwenye uchaguzi wa mitaa jambo ambalo litafanya watu wengi ambao hawakujiandikisha sasa kupoteza haki yao ya kupiga kura.
Andengenye amesema hayo katika kituo cha kujiandikisha cha kata ya Kigoma alipojitokeza kujiandikisha katika daftari la wakaazi wa mtaa wa Shede Manispaa ya Kugoma Ujiji na kuwataka wananchi wa kutumia vizuri siku chache zilizobaki kutimiza haki yao ya kikatiba na kisheria ya kujiandikisha.
Amesema kuwa ni vizuri wananchi kuwa waangalizi wa uchaguzi huo katika maeneo yao kwa kuwatambua na kuwafichua raia wa nje ambao hawana sifa ya kuandikishwa kuwa wapiga kura.
Akieleza muitikio wa watu kujitokeza kujiandikisha katika zoezi hilo kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa amesema kuwa zoezi lilianza kwa kusuasua lakini wameoongeza juhudi ambazo wanaamini zitawezesha kufikia lengo la uandikishaji lililowekwa.