RC Makalla akutana na Balozi Mdogo wa Kenya

MKUU wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amekutana na kuzungumza na Balozi Mdogo wa Kenya mkoani humo Balozi David Maina, wakikubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano ya pande hizo mbili kupitia mpaka wa Namanga ili kukuza uchumi, biashara na Utalii kupitia mpaka huo unaounganisha Tanzania na Kenya.

Balozi Maina aliyefika ofisini kwa RC Makalla kujitambulisha kufuatia uteuzi wake hivi karibuni, amempongeza Makalla kwa kuendelea kuimarisha usalama na biashara kwenye mpaka wa Namanga, akirejea ziara yake ya hivi karibuni alipotembelea eneo hilo na kuzungumza na wananchi wa Tanzania na Kenya wanaoishi na kufanya biashara katika eneo hilo.

“Sisi na Tanzania hatuna shida yoyoye na ile ziara yako pale Namanga ndiyo imefanya niamue kuja kujitambulisha kwako, ulifanya kazi nzuri sana kusisitiza kuhusu amani na kujiridhisha kuhusu usalama. Ulitoa majibu ya maswali mengi sana ambayo Kenya tulikuwa tunayapokea na mpaka leo tunatumia ile hotuba yako kuwahakikishia wananchi usalama,”amesema Balozi Maina.

Katika mazungumzo yao, RC Makalla ameutaja mpaka huo na Kituo cha pamoja cha forodha Namanga kama kiungo muhimu cha uchumi wa Kenya na Tanzania, akihimiza umuhimu wa kutunza ujirani mwema, kulinda amani na kukuza biashara miongoni mwa wananchi wa pande hizo mbili.

Viongozi hao kadhalika wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kuondoa vikwazo mbalimbali vitakavyojitokeza, wakisema ushirikiano wao huo wa pamoja umedhamiria kusaidia kutekeleza ndoto za wakuu wa nchi za Tanzania na Kenya kuhakikisha wananchi wananufaika kiuchumi na kijamii kupitia mpaka huo kwa kubadilishana bidhaa, huduma na watalii wanaoutumia mpaka huo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button