RC Makalla : Utalii Arusha wazidi kuimarika

MKUU wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, ameongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Mkoa wa Arusha, ambapo wajumbe wa kikao hicho wamejiridhisha kuwa shughuli za utalii zinaendelea vizuri, huku idadi ya watalii ikiendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani humo.

Katika kikao hicho, Makalla amekishukuru  Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO) kwa ushirikiano wao na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakati wa tukio la uvunjifu wa amani lililotokea Oktoba 29, 2025, pamoja na mchango wao endelevu katika kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa.

Hatahivyo amesema Mkoa wa Arusha upo katika hali ya utulivu na amani, hivyo kuwataka watalii na wageni wengine kuendelea kutembelea vivutio kama Hifadhi ya Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, Serengeti na Tarangire. Amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama itaendelea kulinda vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Arusha na kuhakikisha usalama wa watalii wakati wote.

Katika hatua nyingine, amezielekeza Wilaya zote sita za Mkoa wa Arusha kuimarisha usalama katika maeneo yao, kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na maandalizi ya msimu mpya wa masomo na kilimo unaotarajiwa kuanza Januari 2026. SOMA: Mutafungwa “ulinzi na usalama ni jukumu la kila Mwananchi”

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button