RC aagiza tingatinga mbovu itengenezwe

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Suleiman Msumi kuhakikisha tingatinga la kutengeneza barabara iliyokaa bila kutengenezwa inafanya kazi mara moja ili kuondoa kero ya barabara.

Mongella ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya elimu, barabara na maji katika halmashauri hiyo na kubaini barabara ni mbovu zenye zumbi lililo kama unga na kuleta adha kwa wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi waendapo shuleni.

Amesema barabara zilizopo halmashauri hiyo ni mbovu hali inayosababisha wananchi kulalamika, huku mitambo iliyopo ikiwa imeota kutu kwa kisingizio cha kupeleka invoice kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) kutengenezwa, lakini hadi sasa Temesa hawajaja kutengeneza katapila hilo.

“Barabara zenu ni za hovyo sana, shuleni pale Mringa, na hata tulipopita huko barabara ni vumbi tu hivi mnategemea wananchi wanaionaje serikali,yani hamtengenezi barabara hili ligari limekaa hapa mnasema mnatengeneza bajeti mwakani huku barabara zenu ni vumbi tu”

 

Habari Zifananazo

Back to top button