RC Mtwara ataka wananchi wawezeshwe fursa Nanenane

LINDI; MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawal,a amewataka wakurungezi watendaji na viongozi wa wilaya za mikoa ya Mtwara na Lindi kuwawezesha wakulima kufika viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kuangalia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi nchini.

Sawala ametoa maagizo hayo leo Agosti 1,2025 wakati akifungua maonesho hayo ya 12 Kanda ya Kusini , 2025 katika Viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi.

“Nisisitize kwa wakurungezi na viongozi wa wilaya zote mikoa ya Lindi na Mtwara kuangalia namna ya kuwawezesha wakulima, wafugaji, na wavuvi kufika katika viwanja hivi kujionea mambo mapya, teknolojia mpya na mbinu mpya kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi,” amesema.

Amewataka viongozi hao kwenda maeneo mbalimbali ya wakulima, wafugaji na wavuvi kuwatangazia kuhusu maonyesho ya Nanenane 2025, ili waweze kujitokeza kwenda kuangalia fursa mbalimbali kwenye sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Katika hatua nyingine, Sawala amewataka wananchi wenye sifa kujiandaa kupiga kura, kudumisha amani wakati wa kampeni na kuhamasisha pia kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wa bungeni na kwenye halmashauri.

Maonesho ya Nanenane 2025 yenye kaulimbiu “Tuchague Viongozi Bora kwa ajili ya Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’ yanafanyika kwa mara ya 32 nchini.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button