MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ameungana na waombolezaji wengine wakiwamo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dk. Batilda Buriani katika maziko ya Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tanga Selemani Sankwa.
Maziko hayo yamefanyika leo Disemba 22,2024 kwenye makaburi msafa yaliyopo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo, yaliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM John Mongela.
Marehemu huyo amefariki Disemba 20, 2024 katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Aidha wakati wa uhai wake marehemu huyo aliwahi kuajiriwa serikalini kabla ya kuajiriwa na CCM kwa nafasi mbalimbali ikiwemo Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Mtwara.