REA waendelea kuhamasisha matumizi nishati safi

DAR ES SALAAM: WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ili ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ya kupikia kama inavyoelekezwa katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034.

Hayo yameelezwa na mhandisi wa miradi kutoka REA, Raya Majallah kwa Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Nishati kutoka Umoja wa Ulaya, Max Pedetti alipotembelea banda la REA, Dar es Salaam.

“Tunaendelea na uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia nyenzo mbalimbali ili kuhakikisha tunafanikiwa kufikisha lengo la 80%,” alisema Raya.

Pedetti alipongeza jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na REA na alisisitiza REA iendelee na utoaji wa elimu ili wananchi watambue umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia.

SOMA ZAIDI: Ajenda nishati safi inavyoibeba Tanzania 

Katika maadhimisho hayo REA kwa kushirikiana na wadau wake imepata fursa ya kuonesha teknolojia za bidhaa mbalimbali za nishati safi ya kupikia, sambamba na kushiriki kikamilifu mijadala mbalimbali kuhusu nafasi ya nishati jadidifu katika kufikia lengo la taifa la kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.

Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu. yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa Idara ya Nishati kutoka Umoja wa Ulaya, Max Pedetti akimwakilisha Balozi wa Umoja wa Ulaya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button