Trump, Putin kukutana wiki ijayo

GENEVA : NAIBU Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Dmitry Polyanskiy, amesema Rais wa Urusi, Vladimir Putin, huenda akakutana na Rais wa Marekani, Donald Trump, wiki ijayo.
Polyanskiy amesema mkutano huo utakuwa wa pili tangu Putin alipokutana na Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, mjini Geneva mwaka 2021. SOMA: Nitamaliza vita vya Urusi na Ukraine – Trump
Hata hivyo, ameeleza kuwa hana taarifa kuhusu mkutano wowote uliopangwa kati ya Rais Putin na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy. Urusi iliivamia Ukraine Februari 2022, ikidai kulinda usalama wake, lakini Ukraine na washirika wake wa Magharibi wamelieleza tukio hilo kama unyakuzi wa mabavu wa ardhi unaoendeleza mfumo wa kikoloni.



