Rombo Marathon kuvuta wanariadha 1000

WANARIADHA  1000 wanatarajiwa kushiriki msimu wa pili wa mbio za riadha za Rombo Marathon zitakazofanyika wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.

Mbio hizo ambazo hufanyika kuelekea sikukuu za Christmas zimepangwa kukimbiwa Desemba 23 mwaka huu.

Zimeandaliwa na Rombo sports Agency zitahusisha mbio za Kilometa 21,Kilometa 10 na Kilometa 5 ambapo zitakimbiwa katika hifadhi ya misitu Rongai kuzunguka Mlima Kilimanjaro.

Akizungumzia maandalizi ya mbio hizo Mratibu wa Rombo Marathon Temy Isdori amesema mbio hizo zinaenda kufanyika kwa msimu wa pili na zinararajiwa kuvuta wakimbiani zaidi ya 1000 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

“Lengo la mbio hizi ni kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo kwa shule za msingi na secondari zilizopo wilayani Rombo pia kuunga mkono ukarabati na ujenzi wa miundombinu katika hospitali ya Huruma ili iwe na hadhi ya mkoa,”amesema Isdori.

Amesema  mbio hizo zitahusisha kilomita 21,Kilometa 10 na Kilometa 5 zitakimbiwa katika hifadhi ya misitu Rongai kuzunguka mlima Kilimanjaro.

Amefafanua zitaanza na kumalizika  katika viwanja vya Michezo vya Misitu ya Rongai vilivyopo Tarakea wilayani humo huku mbio hizo zikihitimishwa kwa mlo wa mbuzi waliochomwa, maarufu kwa jina la ‘Ndafu!’

“Zoezi la usajili linaendelea katika mikoa ya Dodoma,Dar-es-Salaam, na Kilimanjaro ambapo pia tumealika klabu zote za wakimbiaji nchini,pia taasisi mbalimbali za benki ikiwemo NMB na CRDB, taasisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na mashirika mengine yatakuwepo,” ameongeza Isdori.

Habari Zifananazo

Back to top button