RPC Mtwara ataka ushirikiano kukomesha ukatili wa kijinsia

MTWARA: KAMANDA wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, SACP Issa Suleiman amewataka wadau kutoka taasisi mbalimbali mkoani Mtwara kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia ipasavyo masuala ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii ili kuvitokomeza.

Hayo yamejiri wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa wadau mbalimbali wilayani Mtwara kuhusu kuongeza ufanisi wa kushughulika na ukatili wa kijinsia katika jamii, yaliyoandaliwa na shirika lisiyo la kiserikali linalojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii mkoani mtwara (FAWOPA) kwa kushirikana na Aga khan Foundation na serikali ya Canada.

Mafunzo hayo yanalenga kuimarisha mfumo wa rufaa kwa wahanga wa vitendo hivyo, yaliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani yaliyokutanisha makundi mbalimbali wilayani humo ikiwemo dawati la jinsia, viongozi wa kata, maofisa ustawi wa jamii, makungwi na wengine.

‘’Nimefurahishwa mno na malengo na madhumuni ya kikoa hiki  kwa kukutanisha na kimefanikisha mchanganyiko huu, sisi jeshi la polisi tuna madawati yanayoshughulikia kesi za ukatili lakini hatuwezi kufanya peke yetu kuna hatua mbalimbali inaweza ikaanzia kwetu au ustawi wa jamii, daktari na wengine,” amesema Suleiman

Mkurugenzi wa Shirika hilo la Fawopa Baltazar Komba amesema lengo la kikao hicho ikiwemo kujadili namna ya kuwa na mfumo wa rufaa wenye ufanisi na tija unaoweza kusaidia muhanga wa ukatili kupata haki yake.

‘’Kama tunavyojua mtu anayetendewa ukatili anatakiwa aanzie kwenye ngazi ya serikali za kijiji kuja kwa ofisa ustawi wa jamii kwenda polisi na baadae mahakamani kwa ajili ya kupata haki’’amesema Komba.

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Asha Lukanga amesema tatizo la vitendo hivyo ni kubwa kwenye halmashauri hiyo kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya matukio hayo dhidi ya watoto kufanyiana vitendo hivyo   zaidi kuliko ukatili kwa watu wazima.

Mshauri wa Wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Saut tawi la Mtwara, Lilian Mtani amesema kupitia amepata uelewa mkubwa kuhusu rufaa hizo kwani katika chuo hicho vitendo hivyo vipo kwasababu kuna wanafunzi wadogo wanaokuja chuoni hapo ambao wengi wao ni chini ya umri wa miaka 18 hivyo elimu hiyo inawafikia kikamilifu watoto hao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button