Ruwasa yaokoa maisha ya watu 6,300 Inyara

GEITA: WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Geita imefanikiwa kuokoa maisha baada ya kukamilisha mradi maji na kuboresha huduma ya maji safi kwa wananchi wapatao 6,364 wa kijiji cha Inyara.

Mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya Sh milioni 463.97 huku chanzo cha fedha kikiwa ni fedha za mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambapo hadi sasa wananchi wanahudumiwa kupitia vituo vya kuchotea maji Majumbani 36.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Geita, Mhandisi Sande Batakanwa ametoa taarifa ya mradi huo katika hafla ya uwekeza wa jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi mbele ya viongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2025.

Mhandisi Batakanwa amesema mradi ulianza kutekelezwa mwezi Disemba 2021 na kukamilika mwezi Juni 2023, chini ya mkandarasi aitwaye PET Cooperation LTD ambapo kwa sasa mradi umekamilika, kukabidhiwa na unatoa huduma.

SOMA ZAIDI

Ruwasa wajipanga kupunguza adha ya maji Geita

“Mradi unajumuisha ujenzi wa tenki moja lenye ujazo wa lita 225,000, ukarabti wa nyumba ya mitambo ya kuendesha pampu, ufungaji wa pampu ya kusukuma maji lita 15,970 kwa saa” amesema Mhandisi Batakanwa.

Amesema pia kuna mtandao wa bomba wenye urefu wa Km 13.82 pamoja na ujenzi wa vituo 11 vya kuchotea maji na Chanzo cha maji ni kisima kirefu chenye kina cha mita 120 na uwezo wa kuzalisha maji ni lita 16,000 kwa saa.

Mhandisi Batakanwa amesema mradi umepunguza vifo na magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama kama vile kuhara, homa ya natumbo na kipindupindu.

Amesema pia mradi huo mepunguza muda uliokuwa unatumika kufuata maji mbali ambapo sasa muda huo utatumika kufanya shughuli nyingine za uzalishaji na maendeleo kwa jamii.

“Mradi huu umefungua fursa za kiuchumi ikiwemo uendeshaji wa viwanda vidogovidogo vya kusafisha dhahabu, kufyatua tofali, bustani za miti na mbogamboga”, ameeleza Mhandisi Batakanwa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi ameipongeza Ruwasa na kueleza huo ni mwendelezo wa juhudu za serikali kujali na kulinda uhai wa watanzania kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma bora.

Ussi amegiza viongozi kushirikiana kikamirifu na wananchi kutunza na kuendeleza mradi huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha huduma za kijamii kwa maeneo ya mjini na vijijini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button