Rwanda,Marekani wakubaliana kumaliza mgogoro Congo

RWANDA : RAIS wa Rwanda Paul Kagame amesema amekubaliana na serikali ya Marekani ya kusitisha mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika mazungumzo hayo, Kagame hakuashiria kusalimu amri kufuatia wito wa kuondoa wanajeshi wa Rwanda na waasi wa M23 kwenye mji wa Goma.
Kwenye mazungumzo ya simu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio alimshinikiza Rais Kagame kusitisha mara moja mapigano huku akielezea wasiwasi wake baada ya waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda kuingia Goma.
Kagame aliandika kupitia ukurasa wa X kwamba, amekuwa na mazungumzo yenye tija na Rubio kuhusu umuhimu wa kuhakikisha mapigano yanasitishwa Mashariki mwa Congo pamoja na kushughulikia mara moja kiini cha migogoro.
Marekani kwa muda mrefu imeoinya Rwanda kuhusiana na hatua yake ya kuwaunga mkono waasi wa M23.
SOMA: Waandamanaji Congo wachoma moto jengo la ubalozi wa Kenya
Hivi sasa waasi wa M23 wameingia ndani zaidi ya mji wa Goma na kuchukua udhibiti wa uwanja wa ndege.



