SADC ijipange vyema kukabili changamoto za usalama

HATUA ya Tanzania kuzikumbusha na kuzihimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu umuhimu wa kuimarisha mikakati ya kukabili changamoto za usalama ni ya kupongezwa na imekuja wakati muafaka.
Katika dunia ya leo, uhalifu wa kimataifa na kikanda kama uhalifu wa mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu, biashara ya dawa za kulevya na wizi wa magari siyo tu tishio kwa mataifa binafsi bali ni changamoto ya pamoja inayohitaji suluhisho la pamoja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo alitoa wito huo muhimu wakati akifungua kikao cha Kamati ya Kudumu ya Makatibu Wakuu wa SADC Dar es Salaam.
Kauli yake kwamba changamoto hizo zinaweza kuathiri utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya SADC ya 2050 ni angalizo linalopaswa kuchukuliwa kwa uzito na wanachama wote.
Ni dhahiri kuwa hakuna maendeleo ya kweli yatakayopatikana bila kuwepo kwa amani na usalama wa kudumu. Hali ya ukosefu wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni mfano halisi wa changamoto hiyo.
Tunapongeza jitihada za SADC kwa kupeleka kikosi cha SAMIDRC tangu mwaka 2023 kusaidia juhudi za kurejesha amani nchini humo.
Vilevile, tunashukuru ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na SADC kupitia mchakato wa Luanda na Nairobi unaolenga kuunganisha nguvu za pamoja kurejesha utulivu DRC.
Mkutano huo wa maandalizi ya kikao cha Mawaziri wa Siasa, Ulinzi na Usalama unatoa nafasi muhimu ya kutathmini maamuzi ya Lusaka na kujenga mkakati madhubuti wa kuhakikisha demokrasia, utawala bora na usalama vinatawala ukanda huu.
Hii ndiyo njia pekee ya kulinda mafanikio ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo SADC imeyafikia. Kauli ya Mkurugenzi wa Asasi ya Siasa na Usalama SADC, Profesa Kula Ishmael kuhusu athari za mabadiliko ya kisiasa duniani hasa uhusiano kati ya Afrika na Marekani inatufumbua macho kuwa ukanda wetu hauko salama kisiasa wala kiuchumi iwapo hautakuwa na msimamo wa pamoja.
Kwa msingi huo, tunazisihi nchi wanachama wa SADC kuendeleza mshikamano, kuwekeza zaidi katika usalama wa pamoja na kuhakikisha kila taifa linatimiza wajibu wake katika kulinda ukanda wetu dhidi ya uhalifu wa kimataifa.
Tunatambua kuwa kwa kufanya hivyo, siyo tu tunalinda amani na utulivu bali pia tunafanikisha ajenda ya maendeleo endelevu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
I started using this remote work platform about a month ago, and honestly, I was surprised how simple it is. I’m now making 1170+ per week — just from my phone. No special skills, no interviews. If you’re looking for something real and flexible, I’ve shared all the info on my site.
HERE☛ rb.gy/uvl61c
I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.
This Is Where I Started……….www.get.money63.com

HERE——>>> rb.gy/uvl61c
Safi sana na hongera