Samia aahidi kicheko kwa wavuvi

KAGERA: MGOMBEA wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuboresha sekta ya uvuvi endapo atapewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Akizungumza leo Oktoba 15, 2025 katika mkutano wa kampeni unaofanyika Muleba, mkoani Kagera, Dk. Samia amesema serikali yake itawekeza katika usindikaji wa mazao ya uvuvi ili kuwawezesha wavuvi kunufaika zaidi na kazi zao.

Samia ameeleza kuwa mpango huo utatekelezwa sambamba na kuwapatia wavuvi boti za kisasa kwa mikopo ili kuongeza tija katika shughuli za uvuvi, huku akibainisha kuwa hatua hizo ni sehemu ya mkakati wa serikali wake unaolenga kuanzisha na kuendeleza Kongani za viwanda nchini, ambapo sekta ya uvuvi itapewa kipaumbele ili kuongeza thamani ya mazao na kutoa ajira kwa wananchi.

“Tunapoenda mbele mkitupa ridhaa yenu, katika mkakati wetu wa kuanzisha na kuendeleza Kongani za viwanda, tutaliangalia pia suala la usindikaji wa mazao ya uvuvi ili wavuvi wapate manufaa zaidi sanjari na kuwaletea wavuvi boti za kisasa za mikopo ili wavue samaki zaidi,” amesema Samia.

Samia yupo Muleba kwa ajili ya kuendelea kunadi sera na ilani ya CCM pamoja na kuomba kura za ushindi kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 29, 2025. Kampeni hiyo inalenga kuwafikia wananchi wa maeneo mbalimbali ili kuwahamasisha kushiriki uchaguzi na kufanya maamuzi kwa mujibu wa sera zinazowagusa moja kwa moja.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $100 to $500 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily 💵$20k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…

    Here is I started.→→→→→→→→→ https://Www.Works6.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button