Samia afanya uteuzi viongozi mbalimbali

DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi katika taasisi mbalimbali za umma kutokana na baadhi ya viongozi kumaliza muda wa kuhudumu huku wengine wakiendelea kwa awamu nyingine.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 12, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, ambapo imeeleza kuwa Rais Samia amemteua Dk Ismael Kimirei kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kwa kipindi cha pili.

Aidha, Balozi Ernest Mangu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), akiendelea kwa kipindi cha pili cha uongozi.

Wakati huohuo, Dk. Marina Njelekela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), akichukua nafasi ya Prof. Charles Mkony, aliyemaliza muda wake.

Katika mabadiliko mengine, Juma Fimbo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), huku Prof. James Mdoe akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Prof. Mdoe anachukua nafasi ya Dk. Andrew Kitua, ambaye amemaliza muda wake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button