Samia aiagiza nishati kupitia sera usafirishaji mafuta

RAIS Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Nishati kufanya mapitio ya sera ya usafirishaji wa mafuta nchini ili kuziwezesha kampuni zinazosambaza mafuta ukanda wa Kaskazini kutumia Bandari ya Tanga kupitia GBP.
Rais Samia ameyasema hayo leo machi 1, 2025 wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa ghala la kupokelea gesi ya kupikia ya LPG katika kampuni ya BGP ikiwa ni mwendelezo wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
“Hii kazi wanaifanya vizuri sana wao kama GBP, lakini wale ambao wanachukua mafuta kwa ajili ya usambaza ukanda huu, au kupeleka nje ya nchi kupitia kaskazini bado wanachukulia mafuta Dar es Salaam, nendeni mkafanye mapitio ya sera,” amesema Samia.
Rais Samia amesema GBP Tanga ina mafuta ya kutosha kusambaza kanda ya Kaskazini pamoja na nchi ukanda wa kasikazini hivyo hakuna sababu ya wasambazaji hao wa mafuta kuyachukulia Dar es Salaam.

Aisha, Rais Samia ameipongeza GBP kwa hatua iliyochukua ya kuanzisha vituo vya kujaza gesi kila mkoa na kuongeza kuwa Serikali inaunga mkono uwekezaji huo.
Amewahakikisha wawekezaji serikali kuweka sera rafiki na endelevu zitakazotabirika na sera zitakazowawezesha wawekezaji wa Tanzania kuwa washindani katika soko la ndani na soko la kimataifa.
Awali Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga kabla ya kumkaribisha Rais Samia amesemaTanga ni muhimu ndani ya sekta ya nishati kwani ndio kitovu cha kupokea na kusambazaji wa mafuta Mikoa ya Kaskazini na nchi za Ukanda wa Kasikazini.
“Wenzetu wa GBP ni washirika wa kiuchumi wa sekta ya nishati hususani kwenye sekta ndogo ya mafuta kwa sababu maghala yao ndio yanatumika kupokea na kusambaza mafuta kwa upande wa Kaskazini”. amesema Kapinga.



