Samia apaisha watalii, mapato Selous

JUHUDI za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya Tanzania: The Royal Tour zimeongeza idadi ya watalii katika Pori la Akiba la Selous na kupandisha mapato kufikia Sh bilioni 9.1 kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Ofisa Mhifadhi Daraja la II na Ofisa Utalii Pori la Akiba Selous, Stephano Lukumay amebainisha hayo hivi karibuni alipozungumza katika Kituo cha Kingupira wilayani Rufiji wakati wa kumuaga mtalii aliyetembelea pori hilo, Mmarekani Hyk Aleksanyan.

Lukumay alimshukuru Rais Samia kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ambayo ndiyo inasimamia pori hilo, kwa juhudi zake zilizochangia mafanikio hayo.

Akifafanua kuhusu mafanikio hayo, Lukumay alisema kupitia filamu ya Tanzania: The Royal Tour, idadi ya watalii wanaotembelea pori hilo kwa utalii wa uwindaji imeongezeka kutoka watalii 104 mwaka 2021/2022 hadi watalii 245 mwaka 2024/2025.

Aidha, alisema kwa ongezeko hilo mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 3.5 hadi Sh bilioni 9.1 katika kipindi hicho.

“Ni jambo la kipekee na tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea wageni
wengi zaidi katika Pori la Akiba Selous,” alieleza Lukumay.

Kwa upande wake, Aleksanyan ambaye alitembelea pori hilo kwa utalii wa uwindaji, alionesha furaha yake kwa kufanikiwa kuua simba ambaye anasema hajawahi kumpata mahali kokote alikowahi kutembelea isipokuwa Selous.

“Nimekuja nimekuja katika pori zuri la Selous Tanzania kwa ajili ya uwindaji halisi wa wanyamapori. Tanzania ni
nzuri, nimekuwa katika nchi nyingi za Afrika lakini Tanzania inaonekana kuwa ndiyo iliyonivutia zaidi,” alisema
Mmarekani huyo.

Aliongeza: “Kama nilivyosema kuna wanyamapori halisi hakuna vijiji, ni eneo lenye wanyamapori tu. Nimekuwa na siku 21 hapa, ni siku nzuri zenye uzoefu wa kutosha, tumewinda sana, tumekuwa na siku ndefu za kutosha, tumekuwa tukitumia saa 16 kwa siku tukitafuta na kuwinda Wanyama. Tulijitahidi kwa nguvu zote kutafuta simba”.

Aliwahamasisha raia wenzake wa Marekani waje na wafurahie kuona wanyamapori halisi na kuongeza kuwa Tanzania ni nchi nzuri na ya kustaajabisha hivyo watafurahi uwepo wao katika nchi hii.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I started using this remote work platform about a month ago, and honestly, I was surprised how simple it is. I’m now making 1170+ per week — just from my phone. No special skills, no interviews. If you’re looking for something real and flexible, I’ve shared all the info on my site.

    HERE☛ rb.gy/uvl61c

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button