Samia awaahidi watahiniwa Kidato cha Sita

DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan amewatakia heri wanafunzi wote wa Kidato cha Sita ambao wameanza mitihani yao leo ya kuhitimu Kidato cha sita

Rais Samia ametoa pongezi hizo kupitia ukurusa wake wa Instragram leo Mei 6, 2024 akiambatanisha na dua ya mafanikio katika hatua zinazofuata

Rais Samia Suluhu Hassan

“Nawatakia kila la kheri wanafunzi wote wa Kidato cha Sita mnaoanza mitihani yenu ya kuhitimu elimu ya sekondari leo. Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awafanikishe katika hatua hii kwa mafanikio na kila jema katika hatua zinazofuata,” amesema Rais Samia.

https://habarileo.co.tz/samia-awaahidi-watahiniwa-kidato-cha-sita/

Aidha,Rais Samia amesema ana imani kuwa muda wao wametumia vyema kujiandaa,hasa baada ya serikali kuamua kufuta ada kwa kidato cha kwanza hadi cha sita na kuboresha shule zaidi,Ujenzi wa mabweni sehemu ambazo ni hatarishi hasa kwa watoto wa kike

“Nina imani kuwa mmetumia muda wenu shuleni kujiandaa vyema, hasa baada ya Serikali kuamua kufuta ada kwa Kidato cha Kwanza hadi cha Sita, kujenga na kuboresha shule zaidi, ujenzi wa mabweni sehemu ambazo wanafunzi, hasa wa kike, walikuwa kwenye mazingira hatarishi na kuongeza Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Uamuzi huu umeleta nafuu na faraja katika familia nyingi na ongezeko la watahiniwa zaidi kutoka 106,883 mwaka jana hadi 113,504 mnaoanza mitihani leo,” amesema Rais Samia.

Pia,Rais Samia amesema  Hatua wanayoanza leo ya elimu ni muhimu katika kuleta mchango katika maendeleo ya Nchi kwa siku Zijazo kutokana na vipawa,Juhudi na kujituma kwao

“Hatua mnayoanza leo ni muhimu katika safari yenu ya elimu na tunategemea vipawa, juhudi na kujituma kwenu kuleta mchango katika maendeleo ya nchi yetu kwa siku zijazo. Ahadi yangu ni kuendelea kufanya kazi, kupanga na kutekeleza mipango na sera ambazo zitawawezesha kutimiza nia yenu ya kuwa wananchi wenye mchango mkubwa kwa jamii na taifa letu ikiwemo; kuongeza fungu kwa wanafunzi zaidi kupata mikopo ya elimu ya juu na kuboresha sera na mazingira ya kukua kwa sekta binafsi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuzalisha ajira nchini.” amesema Rais Samia.

Habari Zifananazo

Back to top button