DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan leo anaongoza Watanzania katika maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashajaa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewaomba wakazi wa Dodoma wahudhurie maadhimisho hayo katika mji wa serikali Mtumba.
SOMA: https://www.modans.go.tz/events/9
Mnara wa mashujaa umejengwa katika mji wa serikali baada ya kuondolewa mjini kwa maelekezo ya Rais Samia kwamba uhamishwe na ujengwe mahali pengine kwenye nafasi kubwa.
Maadhimisho ya mwaka huu yatakuwa ya pili kufanyika katika Uwanja wa Mashujaa katika mji wa serikali Mtumba. Julai 25 kila mwaka taifa linawakumbuka Watanzania waliopigania, kutetea na kulinda uhuru wa nchi.
Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa hutanguliwa na uwashaji wa Mwenge wa Mashujaa usiku saa sita na kazi hiyo hufanywa na mkuu wa mkoa.
SOMA: Samia mgeni rasmi Siku ya Mashujaa
Wakati wa maadhimisho ya mwaka jana Rais Samia aliwataka Watanzania wasikubali kugawanyika na akahimiza amani, umoja na utulivu wa nchi. “Kamwe, kamwee tusikubali mtu yeyote au kikundi cha watu kutugawa kwa kisingizio chochote kile. Tanzania ni moja na kamwe haitagawanyika,” alisema Rais Samia.
Aliongeza: “Ndugu zangu nimalizie kwa kutoa wito kwa Watanzania wenzangu wote kuwaenzi mashujaa wetu kwa kudumisha amani, umoja, mshikamano na utulivu wa nchi yetu na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu