Samia: Nimemuenzi Magufuli

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema amemuenzi Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Samia amesema anakamilisha miradi yote iliyoanza wakati wa uongozi wa serikali hiyo kumuenzi kiongozi huyo. Amesema hayo wakati wa mkutano wa kampeni Chato.  Chato ni nyumbani kwa Magufuli.

Samia amesema kiongozi huyo alikuwa shupavu na mwenye maono ya kimkakati na ya kimapinduzi.

“Alikuwa ni mwalimu mzuri na mlezi mahiri. Nitaeleza kwa nini ndio maana kazi tuliyoianza awamu ya tano nimeweza kwenda nayo vizuri, kwa sababu alinielekeza vizuri na ndio maana nimeweza,” amesema.

Samia amesema viongozi wengi waliopita walitekeleza mawazo na maono ya Baba wa Taifa Julius Nyerere lakini naye kwa upande wake amekamilisha miradi hiyo na anaendelea kuifanya mingine ili kumuenzi Magufuli.

“Nyote mtakubaliana nami kwamba nimejitahidi sana kuitekeleza dhamira yake na shauku yake ya kuleta mabadiliko ndani ya nchi yetu,” amesema.

Samia amesema Magufuli alimuachia Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) likiwa asilimia 37, amelikamilisha na umeme unazalishwa hapo.

Ameitaja miradi mingine iliyoanza kutekelezwa wakati wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano na ameikamilisha ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kuihamishia serikali Dodoma.

“Leo tayari watu wanasafiri na vipande kadhaa karibu vinajengwa hadi kule Kigoma… aliniachia Daraja la Kigongo
Busisi likiwa asilimia 21 leo tunasafiri kwa dakika tano sijui saba kutoka huku mwanzo kwenda mwisho kuvuka,
jambo linalotufungulia kanda hii (Kanda ya Ziwa) kuwa kanda ya biashara kwenda nchi jirani,”amesema Samia.

Ameongeza: “Lakini aliniachia suala la kuhamia Dodoma. Kama mnavyojua bunge lilihamia mapema Dodoma,
serikali tumewahi kwenda Dodoma na yeye (Magufuli) akiwepo lakini tunavyozungumza leo tayari mhimili wa tatu wa dola mahakama wenyewe uko Dodoma. Lakini pia, ule mji wetu wa Magufuli City mji wa serikali unakamilika”.

Samia ametaja mradi mwingine ni Mradi wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP) linalotoka Hoima nchini Uganda mpaka Chongoleani mkoani Tanga ambalo sasa liko karibu kukamilika.

“Tumemaliza miradi mingi ya kitaifa ambayo nilianza nayo. Namshukuru Mungu nimefanikiwa kuimaliza na namshukuru yeye (Magufuli) kwa maono yake aliyokuwa nayo kwa wakati ule, kuanza miradi ile na kunifanya mimi niweze kuikamilisha,” amesema.

Alisema katika kumuenzi Magufuli, aliacha hospitali ya kanda ya rufaa ikiwa ndio imeanza lakini walijitahidi na kuleta Sh bilioni 44.4 na kuimaliza kabisa.

“Mpango wetu pia ni kuifanya hospitali hii ya kanda kuwa kituo cha umahiri wa tiba za kibingwa na kibobezi kwa magonjya ya moyo kwa kanda hii ambayo inakwenda pia kuwasaidia wagonjwa wa Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Kagera na Kigoma na pengine nchi jirani wote watakuja hapa kufuata matibabu hayo,” amesema.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button