Odemba: Mikakati, fursa zaja Sauti ya Mitindo

DAR ES SALAAM: JUKWAA la Sauti ya Mitindo Tanzania limejipanga kufanya makubwa kwa mwaka 2026, ikiwemo kuchagua wanamitindo wenye vigezo ambapo kati yao watatu watapewa kazi mataifa ya nje, lengo likiwa kukuza sekta ya mitindo nchini.

Akizungumza leo Novemba 25, 2025, mmiliki wa jukwaa hilo, mwanamitindo nguli, Miriam Odemba ameiambia HabariLeo kuwa mpango huo unalenga kufufua vipaji vya walimwende na kuunga mkono mkakati wa ajira.

“Kama mnavyofahamu kwasasa ni nguli, hivyo lazima niache alama kwa wanamitindo wanaoniangalia kama kioo cha jamii,”amesema Miriam.

Amesema mpango huo pia unalenga kuwashirikisha wabunifu mavazi ili kuangalia namna ya kupata vipaji vipya ili kuwawezesha katika ajira.

“Mpango mwingine ni ‘fashion show’ na kutafuta wadhamini kupitia Miriam Odemba Foundation,” amesema Miriam.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button