Sauti za Busara 2027 kufanyika Machi

TAMASHA la Sauti za Busara linalofanyika kila mwezi Februari kwa mwaka 2027 litafanyika mwezi Machi ili kupisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuwa Februari. Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Journey Ramadhani, amesema tamasha hilo litafanyika kuanzia Machi 11 hadi 14, 2027.
Journey amesema mabadiliko hayo yamelenga kuheshimu mfungo wa Ramadhani, huku akibainisha kuwa tamasha hilo pia litafanyika kwa mara ya pili mfululizo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Zanzibar.Amesema eneo hilo lina nafasi kubwa na linawezesha tamasha kufanyika kwa uhuru zaidi ikilinganishwa na Ngome Kongwe. SOMA: Salif Keita ashindwa kutumbuiza Sauti za Busara
Ameongeza kuwa waandaaji wa tamasha hilo watapeleka mapendekezo mapema kwa Serikali ya Zanzibar ili kuendelea kupewa eneo la Mnazi Mmoja hata baada ya kukamilika kwa maboresho ya Ngome Kongwe, akisisitiza kuwa eneo hilo linafaa zaidi kwa ukuaji na muendelezo wa tamasha hilo.



