NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Hussein Mohammed serikali imewezesha sekta ya kilimo kuwa miongoni mwa sekta za kipaumbele kufuatia kuongezeka kwa bajeti ya kilimo kutoka Sh bilioni 294 kwa miaka mitatu iliyopita mpaka kufikia Sh triliomi 1.2.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameto taarifa hiyo katika kilele cha siku ya mbolea duniani ambacho kitaifa iliyofanyika Oktoba 10-13, 2024 Wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Akizungumzia suala la mbolea, Hussein Mohammed amesema taifa badom lina matumizi madogo ya mbolea kwani Umoja wa Afrika kupitia Mpango wa Mageuzi ya Kilimo ya Afrika wa mwaka 2050 umeelekeza nchi za Afrika ifikapo mwaka 2050 matumizi ya mbolea angalau yawe yamefika kilogramu 50 kwa wakati moja.
“Ili kuweza kuimarisha upatikanaji wa mbolea lazima pia tuboreshe mifumo yetu ya Tehama hivyo Wizara ya Kilimo inaendelea kuwekeza katika kuhakikisha kuwa tuna mifumo mizuri ya Tehama ya kuweza kupata taarifa mbalimbali,” amesema Mohammed.
Aidha aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI, Mrajisi wa vyama vya Ushirika Tanzania na kampuni za mbolea kuhakikisha vituo vya mauzo ya mbolea vinasogezwa karibu na maeneo ya wakulima.
Siku ya kilele yamefanyika mashindano ya jogging ambapo viongozi na wananchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki.