Sera Msaada wa Kisheria mbioni kutungwa

SINGIDA; SERIKALI ipo mbioni kuandaa Sera ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria itakayoweka misingi ya kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kote nchini.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Juma Homera wakati wa uzinduzi wa kliniki ya huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa bure na serikali, uliofanyika mkoani Singida.
Kliniki hiyo ni mwendelezo wa kliniki ya awamu ya kwanza iliyozinduliwa hivi karibuni mkoani Morogoro.
Dk Homera alisema kliniki hizo ambazo zitaendelea katika mikoa mingine zinalenga kutatua migogoro ikiwemo ya ndoa, ardhi, mirathi na ukatili wa kijinsia kupitia taasisi za serikali zikiwemo Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Alisema sera hiyo itajikita katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utatuzi wa migogoro, kuanzisha na kuendesha madawati ya msaada wa kisheria katika ngazi za halmashauri, kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali kupitia makubaliano.
Lakini pia kuimarisha matumizi ya Teknolo jiaya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kuhakikisha daftari la watoa huduma za msaada wa kisheria linahuishwa na kuwatumia kikamilifu mawakili wa serikali katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria.
“Sera hii itaweka msingi imara wa kuhakiki sha wananchi wanapata msaada wa kisheria kwa ufanisi na kwa wakati,” alisema.
Alisema baada ya Morogoro na Singida, ratiba itaendelea katika mikoa mingine na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi pindi huduma hizo zitakapowafikia katika maeneo yao.
Aidha, Dk Homera ameipongeza RITA kwa utekelezaji wa mpango wa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ndani ya saa 48 za kazi kwa kutumia mfumo wa kidijiti wa e-RITA.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba alisema wizara hiyo imeanzisha kituo cha huduma kwa mteja kinachopatikana kupitia namba 0262160360, ambacho kimekuwa kikisaidia kuongeza uelewa wa jamii kuhusu namna ya kuripotina kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia.
“Hivyo, nitoe rai kwa wananchi wote kuungana kwa pamoja kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia watoto,” alisema. Naye Meneja wa Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka wa RITA, Patricia Mpuya alisema RITA imepokea maombi 122,000 ya vyeti vya kuzaliwa kuanzia Desemba 15, mwaka jana



