Sera ya ardhi yaja na malengo 16 mahsusi

SERA ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 Toleo la 2023 ina lengo la kuhakikisha kuna mfumo madhubuti wa umiliki wa ardhi, usawa katika upatikanaji ardhi, usimamizi na matumizi ya ardhi kwa maendeleo endelevu.

Sera hiyo ina malengo 16 mahsusi likiwamo la kuimarishwa mfumo wa umilikaji na uendeshaji ardhi ili kuwezesha raia wote kuwa na haki sawa ya kupata ardhi na kulinda ardhi ya serikali.

Lengo lingine mahsusi la sera hiyo ni kuwepo uwazi na haki katika utwaaji, ubatilishaji wa milki na ulipaji fidia.

Pia, inalenga kuimarisha mifumo ya usajili wa ardhi na miamala ya milki, kuimarishwa kwa usalama wa milki za ardhi ya kilimo na ufugaji kwa ajili ya matumizi endelevu na kuwezesha matumizi endelevu ya rasilimali ardhi iliyotolewa kwa ajili ya uwekezaji.

Aidha, ina lengo mahsusi la kuimarisha mfumo wa uandaaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi vijijini; kuimarisha mfumo wa uandaaji, utekelezaji, usimamizi na udhibiti wa mipango ya matumizi ya ardhi mijini na kuwa na mfumo unganishi na endelevu wa kutunza kumbukumbu za ardhi na taarifa za kijiografia.

Jingine ni kuimarisha usimamizi wa maeneo nyeti kwa maendeleo endelevu; kudhibiti migogoro ya ardhi na kuimarisha mfumo wa utatuzi; kuimarisha mfumo wa upimaji ardhi na upatikanaji wa ramani na kuwa na mipaka ya kimataifa iliyoimarishwa na salama.

Sera hiyo ina lengo la kuwa na mfumo fanisi wa usimamizi wa thamani na soko la ardhi; kuwa na usimamizi wa ardhi unaozingatia hifadhi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi; kuwa na usawa wa kijinsia katika kupata haki za ardhi na kuimarisha utawala bora katika usimamizi wa ardhi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button