Serikali: Ajira 73 za watalaam wa mazingira mbioni

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amelieleza Bunge kuwa watumishi hao watasambazwa katika taasisi mbalimbali za umma

JUMLA ya wataalam wa mazingira 73 wanatarajiwa kuajiriwa katika mwaka huu wa fedha 2022/23 ikiwa ni miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na changamoto za mazingira.

Akizungumza bungeni leo bungeni, Dodoma leo asubuhi katika kipindi cha Majibu na Maswali, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi amelieleza Bunge watumishi hao watasambazwa katika taasisi mbalimbali za umma.

Watumishi hao watasambazwa katika wizara, idara zinazojitegemea, wakala, sekretarieti za mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hatua za utekelezaji ajira hizi zote zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka huu wa fedha 2022/23.

Ndejembi ametoa maelezo hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Asia Halamga aliyetaka kujua lini Serikali itaajiri wahitimu wa kada ya mazingira waliomaliza katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri amesema: “Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuhakikisha Wahitimu wa Kada ya Mazingira na Kada ya Afya ya Mazingira (Environmental Health Officers) wanaajiriwa ili uimarisha jitihada za kukabiliana na athari za uharibifu wa azingira.”

Akifafanua zaidi, Ndejembi amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22, Serikali ilitoa jumla ya vibali vya ajira 223 kwa kada ya mazingira katika taasisi zipatazo 124 ambapo utekelezaji wa ajira hizo unaendelea.

Ameahidi kuwa jitihada kuajiri wataalam hao ni endelevu kutokana na umuhimu wa suala la utunzaji wa mazingira ikiwa ni miongoni mwa mikakati ya nchi na dunia kwa ujumla ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nasibu
Nasibu
5 months ago

Ahsante kubwa vipi kuhusu wanao jitolea bado wataachwa au watapewa kipaumbele???

Mwanasha
Mwanasha
4 months ago

Tunapata vip ajira kwenye idara hii ya mazingira

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x