Serikali kutoa kipaumbele wanawake, watoto

Serikali kutoa kipaumbele wanawake, watoto

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali itaendelea kutoa kipaumbele kuhakikisha wanawake na watoto wa kike wanapata huduma wezeshi, zikiwemo za afya na elimu, ili kuwezesha kujenga jamii yenye usawa.

Amesema serikali inatambua na itaendelea kuunga mkono jitihada za mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali, ikiwemo kuendelea kutunga kuboresha sera za usimamizi wa usawa wa kijinsia, ili kumuwezesha mtoto wa kike kufikia malengo yake.

Ameyasema hayo  alipomuwakilisha  Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye mkutano juu ya kuwezesha vipaumbele vya wanawake na wasichana katika mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Advertisement

Amesema serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha wanaweka kipaumbele kuwahudumia wanawake wanaoishi na VVU, ikiwemo kuviwezesha vikundi vyao, kutoa elimu pamoja na kuwajumuisha katika ngazi za uamuzi kwenye sehemu za kutolea huduma za afya.

“Wasichana wakipata elimu bora wataweza kuepukana na maambukizi ya virusi vya ukimwi, kuanzia katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla, hivyo ni wajibu wetu kuwekeza kwa watoto wa kike, ili kuwa na jamii yenye mafanikio na usawa katika maendeleo,” amesema na kuongeza:

“Tunapaswa kuwaweka wanawake na watoto wa kike kwenye vipaumbele vyetu, ili kuleta mabadiliko kwa jamii, lazima tusikilize sauti zao, na kuwapa nafasi katika ngazi za maamuzi na uongozi, kwa pamoja tunapaswa kuwawezesha mabinti wa kiafrika kufikia nafasi za uongozi.”

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *