Serikali kuunga mkono kilimo miti ya mianzi

SERIKALI imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za uwekezaji katika kilimo cha miti ya mianzi kutokana na miti hiyo kuwa na soko nje ya nchi pamoja na matumizi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa.

Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo wakati wa uzinduzi wa mradi wa upandaji miti ya mianzi Tanzania ambao utafanyika kwa Mkoa wa Morogoro na Kibaha unaosimamiwa na Kampuni ya Shikana Group kwa kushirikiana na Kampuni ya Silva Terra kutokea nchini Uswizi

Prof. Mkumbo amesema kuwa miti ya mianzi ni miongoni mwa miti bora ambayo ni rafiki kwa mazingira na hupunguza gharama za Mazingira.

Advertisement

“Ni jukumu letu kama Serikali kusapoti na kuunga mkono juhudi za ndogo za kati na kubwa katika kutekeleza Dira yetu,” amesema

Ameongeza kuwa mradi huo utaenda kuchangia maendeleo ya Tanzania katika kutoa ajira kwa vijana kutokana mradi huo kughalimu bilioni 280.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Shikana Group, Amne Saudi amesema kampuni hiyo imekuwa ikisaidia wawekezaji Kutoka nje ya nchi wanaokuja kuwekeza Tanzania.

“Miti ya mianzi ni mitia ambayo ina thamani sana watu wengi hawakifahamu lengo kubwa kwenye uwekezaji kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi na soko ndani ya nchi ni kitu kipya  kengo ni kwamba tutaanza kuuza kwenye soko la dunia ambapo inajulikana na washatumia kwenye ujenzi lakini hata kwenye ndege .

“Mradi huu awamu ya kwanza utatumia Dola milioni 50 kuotesha mianzi hiyo huku awamu ya pili tunatarajia itakuwa milioni 50 pia na  kwa awamu ya kwanza tunatarajia kuajiri vijana 5,000 na awamu ya pili itakuwa vijana 1, 000 mpaka 2,000,” amesema Amne.

Mkurugenzi wa Silva Terra, Carl Lambert amesema miongoni mwa sababu zilizo mfanya kuja kuwekeza Tanzania ni pamoja na uwepo wa mazingira rafiki na amani na utulivu.

Zao la mianzi likitajwa kufikia thamani ya Dola bilioni 7 (Sh17.81 trilioni) katika soko la dunia  ambapo takribani watu bilioni 2.5 kutoka Bara la Asia, Afrika na Amerika ya Kusini wanatumia zao hilo kwa matumizi mbalimbali.