Serikali kuwaunga mkono wadau wa ufugaji

SERIKALI imewataka wadau wa sekta ya ufugaji wa kuku na nyama nyeupe kote nchini kuchangamkia fursa kwa kufanya ufugaji wa kimkakati kwani iko tiyari kushirikiana nao ili kuhakikisha tasnia hiyo inakua na kuchangia katika pato la taifa.
Aidha imewashauri wadau wa kuku nchini kuwa na wivu na tasnia yao kwa kutokuruhusu mtu kuharibu soko la kuku nchini kwa kutoa taarifa zisizofanyiwa utafiti kwa kuwa wamoja na wakali mtu anapogusa sekta yao kwa lengo la kuichafua na kuharibu soko hivyo wahakikishe usalama wa chakula kwenye kutengeneza kuku wasitafute tu faida.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti wakati wa maonesho ya kuku wafugwao na kubainisha kuwa kuwa ni jukumu la wadau kuhakikisha kwamba kuku wanaotengenezwa wanakidhi kiwango cha kimataifa.
Naye mwenyekiti wa chama mwamvuli cha wadau wa tasnia ya kuku wafugwao Mwanamvua Kishamte amesema kuwa kama wadau wanauomba na kuishauri serikali kuanzisha minada ya kuuzia kuku kwa kila halmashauri kama ilivyo kwa mifugo mingine,na pia bidhaa za kuku ziuzwe kwa kutumia mizani na sio kukadiria kwa Macho kama ilivyo sasa.
Takwimu za kimataifa zinaonesha kuwa ifikapo mwaka 2032 kutakua na upungufu wa tani 434000 za nyama nyeupe ikiwemo nyama ya kuku na endapo hakutakua na uwekezaji wa kimkakati kwa kuwa kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya nyama hiyo.