Serikali yaweka mikakati sekta ya kuku

SERIKALI imeahidi kuweka mikakati mbalimbali katika kuhakikisha sekta ya kuku na ndege wafugwao inakua na kuchangia zaidi katika ajira, uchumi na kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Mikakati hiyo ni pamoja na kuanzisha mashamba ya kuku yakiwemo mashamba ya kuku wazazi, uwekezaji katika maeneo ya kutotoleshea vifaranga vya kuku, kuanzishwa kwa kiwanda kipya cha vyakula vya mifugo.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Kilimo Zanzibar, Shamata Shaame wakati wa kufunga jukwaa la Tasnia ya Kuku na nene wafugwao kwa nchi za Kusini kwa Afrika.

Shamata amesema moja ya mkakati mwingine ambao wanatarija kuufanya ni kushirikiana na wadau wa maendeleo, sekta binafsi na wawekezaji ili kuleta mageuzi ya haraka kwenye tasnia hiyo.

“Serikali inatarajia kuanzisha programu za pamoja za utafiti kati ya nchi za SADC ili kushughulikia changamoto zinazofanana zikiwemo udhibiti wa magonjwa, mbinu na teknolojia za kuboresha ufugaji,”alisema

Amesema Serikali itaendeleza programu za mafunzo za kikanda kwa wafugaji, madaktari wa mifugo, na wafanyakazi wa ugani ili kuongeza ujuzi katika usimamizi wa kisasa wa kuku na ustawi wa wanyama.

Habari Zifananazo

Back to top button