Serikali kuwekeza katika teknolojia sekta madini

DAR ES SALAAM: SERIKALI kuwekeza katika teknolojia ya hali ya juu ya tafiti ili kusaidia kupata taarifa za kijiolojia zitakazowezesha kupata taarifa za kina katika sekta ya madini nchini.

Hali hiyo itafanya kushawishi uwekezaji utakaoongeza ufunguzi wa migodi mingi itakayotengeneza ajira nyingi nchini.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 25, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyemuwakilisha katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

Serikali imewataka wadau sekta ya madini kuwekeza katika uchenjuaji, utafutaji, uhifadhi na ufanyaji biashara ya madini kwa kuangalia maslahi ya nchi na watu wake.

Aidha serikali imesema imejipanga kuiwezesha migodi nchini sambamba na wachimbaji wadogo ikiwemo katika upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa kuiunganishia na gridi ya umeme ya taifa.

“Migodi zaidi ya 350 imeunganishwa na gridi ya taifa ya umeme,” amesema Biteko kwa niaba ya Rais Samia.

Aidha amesema serikali imesema itanunua mitambo mingi ili kusaidia wachimbaji wadogo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
SandyLayman
SandyLayman
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by SandyLayman
Marry
Marry
1 month ago

●Im making over $13k a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life.(sj)last month her pay check was $12712 just working on the laptop for a few hours. This is what I do, ↓↓↓↓VISIT THIS WEBSITE↓↓↓↓
HERE☛…..☛ http://Www.Smartcareer1.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x