Serikali kuwekeza vifaa vya kisasa DMI

MKUU wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Dk,Tumaini Gurumo amesema serikali imeona upo umuhimu wa kuongeza jitihada za kuwekeza zaidi katika chuo hicho kwa kununua vifaa vya kisasa vya kufundishia, ili kufungua ajira zaidi kwa watanzania ndani na nje ya nchi.

Akizungumza jijini Arusha katika banda la maonesho la chuo hicho, Dk,Tumaini amesema fursa zipo nyingi kwenye usafirishaji majini,ndani na nje ya nchi,hivyo jitihada za uwekezaji zinazofanyika katika chuo hicho, zitasaidia kuounguza uhaba wa ajira nchini.

Advertisement

“Tunaishukuru serikali kuwekeza fedha nyingi katika ununuzi wa mitambo mikubwa ya kisasa ya kufundishia kutoka nje ya nchi, ambapo mmoja umeshawasili chuoni hapa na mmoja upo njiani kuwasili na vifaa mbalimbali vya utoaji elimu tumenunua,”alisema.

Amesema kwa ujumla sekta ya uchukukuzi na usafirishaji majini kuna fursa kubwa za ajira, kutokana na uhaba wa wataalamu, hali inayosukuma DMI kwa kushirikiana na serikali kufanya jitihada kubwa kuzalisha wataalamu.

“Ambapo kwa sasa chuo hicho kutokana na maboresho mbalimbali yanayofanyika kimefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 8000 hadi kufikia 12,000 mwaka huu,”.