Serikali kuwekeza zaidi sayansi data, akili unde

DODOMA: SERIKALI na Benki ya Exim zinakusudia kufadhili masomo ya wanafunzi wa elimu ya juu wa Sayansi Data na Akili Unde.

Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa benki hiyo kujenga rasilimali watu wenye ujuzi wa teknolojia ya kisasa, sambamba na kusaidia utekelezaji wa mageuzi ya elimu.

Hayo yamejiri katika kikao kilichomkutanisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda na uongozi wa Benki ya Exim kilichofanyika jijini Dodoma leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya kikao hicho, lengo la ufadhili huo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na benki hiyo katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya elimu nchini.

Aidha, uongozi wa benki hiyo ujumbe uliongozwa na Ofisa Mkuu wa Fedha, Shani Kinswaga, akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wa Kati, Andrew Lyimo, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Stanley Kafu.

Wizara ya Elimu imekuwa ikisisitiza umuhimu wa kuwekeza katika masomo ya STEM, na hasa teknolojia za mstari wa mbele, ili kuendana na kasi ya mapinduzi ya nne ya viwanda.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button