Serikali, wadau kushirikiana kuboresha malezi

KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Zainab Chaula ametoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana na serikali kuwahudumia wananchi kwa kuboresha miundombinu ya malezi na miradi itakayosaidia kufikia ustawi wa jamii.

Dk Chaula ametoa rai hiyo wakati akipokea gari lililotolewa na Shirika la PACT Tanzania kupitia mradi wa Achieve ili litumike kuimarisha huduma za ustawi wa jamii hususani uratibu wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Gari hiyo ni miongoni mwa magari matatu yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 236.6 yaliyotolewa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kupitia mradi wa Achieve unaotekelezwa na Shirika la Pact Tanzania ambayo yameelekezwa Ofisi ya Rais-Tamisemi, Wizara ya Afya kwenye Kitengo cha Elimu na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu.

Alisema Serikali inatekeleza majukumu mbalimbali kuhakikisha changamoto katika jamii zinatatuliwa, hivyo kwa kushirikiana na wadau itaharakisha kufikiwa kwa matokeo tarajiwa.

“Kama Serikali tumekuwa na mambo mengi tunatekeleza kuanzia kujengeana uwezo kwa sababu wizara ni mpya, lakini pia kuimarisha miundombinu.

“Sisi kama Wizara tunaendelea kutoa wito kwa wadau wengine wajitokeze ili tuunganishe nguvu kwa pamoja kwani tunamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutoa huduma kwa wananchi,” alisema.

Naye Mkurugenzi mkazi wa Shirika la PACT Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mradi wa Achieve, Levina Kikoyo alisema lengo hasa la kutoa gari hilo ni kuhakikisha mifumo ya serikali inafanya kazi katika utekelezaji wa programu na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali ili ziwafikie walengwa kwa ustawi na maendeleo ya jamii na zinakuwa endelevu.

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x