Serikali yaahidi kuajiri walimu zaidi kukabili upungufu

SERIKALI imekusudia kuajiri walimu zaidi katika mwaka ujao wa fedha ili kuendana na changamoto iliyojitokeza baada ya serikali kujenga madarasa zaidi na ongezeko la wanafunzi shuleni, vyuo vya kati na vikuu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Margaret Musai wakati watafiti wakiwasilisha matokeo ya ‘Utafiti Elimu Tanzania’ yaliyowasilishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana na kusisitiza kwa sasa serikali imejikita kuongeza watumishi wa kada hiyo.

“Unapojenga miundombinu ina maana na idadi ya wanafunzi inaongezeka…hayo ni matokeo mazuri sana ya serikali. Karibu kila mto wa Kitanzania yupo shuleni anasoma. Sasa inakuja changamoto ya walimu,” amesema.

Advertisement

Mkurugenzi huyo amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa za kuajiri walimu ili kuendana na changamoto hiyo huku kipaumbele katika mwaka ujao wa fedha kikiwa ni kuajiri walimu wengi zaidi katika ngazi ya msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na Balozi wa Canada Kyle Nunaz Canada na mwenzake Uingereza David Concur, Mkurugenzi Msaidizi alisema Serikali inapenda kufanya kazi na wadau wanafanya kazi ya kumsaidia mtoto wa Kitanzania.

“Kwa sasa sisi (Wizara ya Elimu) tunafanya maboresho ya Sera ya Elimu ili kutoa elimu iliyo bora na si bora elimu tu. Elimu bora inamwangalia mtoto kuanzia ngazi ya awali, elimu ya msingi, sekondari, katika vyuo vya ufundi na vyuo mbalimnbali hapa Tanzania,” alifafanua.

Katika kufanikisha hilo, Musai alisema, Wizara inapitia rejea mbalimbali na utafiti ili kupata sera inayoakisi mahitaji ya sasa.

Naye mwakilishi wa Mkurugenzi wa Elimu kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Yusuph Singo alikiri aliyeshiriki mkutano huo wa kupokea matokeo ya Utafiti Elimu Tanzania 2023, alikiri umuhimu wa utafiti katika kuboresha sekta hiyo huku akiri licha ya kwamba hakuna matokea bado alikuwa hajayapata, kuna uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na kujifunza kwa wanafunzi.

Naye Faith Shayo, Mkuu wa Kitengo cha Elimu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) alisema kuwa kwa sasa wadau wanaangazia suala la elimu na mabadiliko ya tabia nchi.

Shayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Washirika wa Maendeleo ya Elimu Tanzania kwa sasa jitihada za wadau ni kuifanya elimu iweze kuchangia kufikia maendeleo endelevu.

Watafiti wa masuala ya elimu wameanza kuhusisha kuhusisha athari za mabadiliko ya tabianchi katika elimu huku wakipendekeza kuboresha mazingira ya kujifunzia ili kukabiliana na changamoto hizo.

1 comments

Comments are closed.