Serikali yafunguka ripoti ya uchunguzi ajali ya Precision air

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mlango wa ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyopata ajali ziwa Victoria ikijaribu kutua Bukoba ulifunguliwa na mhudumu akisaidiana na abiria.

Akitoa ripoti ya uchunguzi wa ajali hiyo, Waziri Mbarawa amesema wavuvi walifika katika eneo la ajali hiyo mwendo wa dakika tano tangu itokee na kwamba jitihada za wao kujaribu kufungua mlango ziliwaongezea ari mhudumu na abiria kufungua mlango.

Mbarawa amesema hali ya hewa ilibadilika ghafla na boti ya uokozi ilichelewa kwa kuwa ilikuwa doria. Ripoti hiyo kwa mujibu wa Waziri anayehusika na uchukuzi haikutaja majina.

“Ni kweli mlango ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa msaada wa abiria, hata hivyo kama ripoti ya uchunguzi inavyosema wananchi waliokuwa wanafanya shughuli za uvuvi walifika eneo la ajali dakika 5 baada ya ndege kuanguka,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button