Serikali yaihudumia Stars asilimia 100

TANGA; RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), amesema timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu (Taifa Stars) inayoshiriki fainali za CHAN 2024, inahudumiwa na serikali kwa asilimia 100.
Akizugumza baada ya kuthibitishwa kuwa Rais wa TFF kwa miaka minne ijayo leo Agosti 16. 2025 jijini Tanga, Karia aliishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikitoa kwa TFF katika kuhakikisha mambo yanaenda.
Amesema kutokana na nguvu hiyo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Dk Samia Suluhu Hassan, wachezaji wa Taifa Stars walilipwa posho zao hadi za leo Agosti 16 na kwamba posho nyingine za mechi zijazo nazo hadi kufikia Jumatatu watakuwa wamelipwa.



