Serikali yapewa ushauri athari uamuzi wa Trump

SERIKALI imeshauriwa kutenga bajeti ya ziada kugharimia programu zilizokuwa zikifadhiliwa na serikali ya Marekani ili wananchi wasikose huduma zikiwemo za afya.
Aidha, Bunge limeombwa kujadili kwa dharura uamuzi wa Serikali ya Marekani wa kuzuia misaada kwa nchi masikini ikiwemo ya afya na liishauri serikali kwa manufaa ya nchi.
Miongoni mwa waliozungumza na gazeti la HabariLEO juu ya suala hilo, ni Mhadhiri kutoka Shule ya Biashara Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Omary Mbura amesema taifa linapaswa kutafuta njia mbadala kugharimia huduma zikiwemo za afya ziendelee kupatikana miongoni mwa wananchi.
Profesa Mbura amesema serikali inapaswa kugharimia au kupata dawa hizo kutoka sehemu nyingine na iwatoe hofu wananchi hususani wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
Mchambuzi wa masuala ya uchumi, Walter Nguma amesema nchi za Afrika zinapaswa kuwa na bajeti inayokidhi mahitaji ya kununua afua za afya kwa kutumia rasilimali zao.
“Hatua ya Marekani itutoe usingizi Waafrika, tunategemea hadi chandarua, hii ni aibu na tutegemee kupata manyanyaso. Tuanze kutekeleza dhana ya kujitegemea kwa vitendo na si maneno,” amesema Nguma.
Amesema ni muhimu Bunge la Tanzania likajadili suala hilo kwa sababu kama nchi haikuwa na bajeti ya kununua dawa liishauri serikali jambo la kufanya.
“Suala hili lichukuliwe kwa udharura wake kwa kutenga bajeti itakayokuwa maalumu kwa ununuzi wa dawa na si kuendelea kutegemea misaada inayotufanya kuwa watumwa, badala yake tuone ni jukumu letu hata kama watabadili maamuzi,” amesema Nguma.
Mchambuzi wa uchumi, Gabriel Mwang’onda amesema kama Tanzania ilivyoweza kutoa huduma ya usambazaji umeme katika vijiji vyote kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na bila kutegemea ufadhili, inaweza kusimama yenyewe na kupata dawa hizo.
“Wizara ya Afya ina dawati la dawa za asili, ni wakati wa kutoa fedha kwa watafiti wetu waweze kufanya utafiti kupata dawa za asili ambazo zitatumika kufubaza VVU na kutibu malaria badala ya kutegemea dawa kutoka nje,” amesisitiza mchambuzi huyo wa uchumi.
Mchambuzi wa masuala ya diplomasia, Goodluck Ng’ingo amesema uamuzi wa Marekani unazikumbusha nchi za Afrika umuhimu wa kuwa na viwanda vya kutengeneza dawa.
“Kwa sababu ARVs hazitengenezwi Marekani, zinatengezwa India, Marekani wanasaidia kutoa fedha kuzinunua kwa ajili ya nchi masikini ambazo zina uwezo wa kutengeza viwanda,” amesema Ng’ingo.
Dk Cecilia Makafu amesema ni wakati wa serikali kufanya jitihada za haraka kunusuru hali hiyo kabla ya madhara kuwapo.
“Tatizo lipo kweli kwa maana baada ya zile dawa za akiba ambazo huwa zinakuwepo, kwa kawaida zikiisha maana yake ugonjwa utafumuka, kama tulikosea mwanzo basi tuangalie tulipoishia turekebishe,” amesema Makafu.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya amehimiza serikali kufanya jitihada kunusuru afya za wananchi.
“Ukimwi upo, polio, kifua kikuu, matende vyote vipo ila tu havionekani kutokana na kinga na tiba tulizokuwa tunapata kwa hiyo serikali ione itasaidia vipi wananchi wake,” amesema Sakaya.
Aliongeza: “Tulishasahau kama kuna Ukimwi tukawa tunashughulika na magonjwa mengine ambayo kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa, sasa turudi tena kwenye kupambana na huu ugonjwa tusisubiri mpaka vifo. Hii ni kengele tufanyie kazi,” amesema.
Takwimu zinaonesha Ukimwi bado ni tatizo duniani. Kwa mujibu wa WHO, hadi mwishoni mwa 2023, watu milioni 39 duniani walikuwa wanaishi na VVU.
Technická řešení nová kasina 2025
Skupina n. v. jsme pro vás připravili celý zajímavý Informace o zahraničních kasinech, působící na českém online trhu.
Nếu bạn đam mê cá cược thể thao, hãy thử thể thao fly88, giao diện dễ theo dõi, tỷ lệ cao.
brilliant web publication article. I’m going to bookmark and read much more
often. I adore the blog template