Serikali yashauriwa kuwatambua wafanyabiashara wadogo kwa ajili ya kodi

DAR-ES-SALAAM : SERIKALI imeshauriwa kuanzisha utaratibu mzuri wa kuwafahamu wafanyabiashara wadogo nchini ili waweze kuingizwa katika mifumo rasmi ya ulipaji wa kodi.

Pendekezo hili limetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, ambaye amesema ni muhimu kwa wafanyabiashara hawa kutambulika ili waweze kuchangia mapato ya serikali kwa mujibu wa sheria.

Akizungumzia kwa undani kuhusu wafanyabiashara wadogo ambao kwa sasa wanafikia milioni nane, kulingana na takwimu za Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Issa amesema licha ya kuwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara wadogo wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo, wengi wao bado hawatambuliki katika mifumo rasmi ya ulipaji wa kodi.

“Wafanyabiashara wengi wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo, lakini kutokana na kutokuwa na utaratibu wa kuwaatambua, wengi wao hawajui haki zao na wajibu wao katika ulipaji wa kodi, jambo linalochangia kukosekana kwa mapato ya serikali,” alisema Issa.

SOMA:Dk Mwinyi awapa raha wafanyabiashara wadogo

Aidha, Issa ametoa pendekezo maalum kwa serikali kuangalia njia bora ya kutambua wafanyabiashara hawa kuanzia mijini hadi vijijini, ili waweze kuwa sehemu ya mifumo rasmi ya kodi, hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa taifa na ustawi wa serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button