Dk Mwinyi awapa raha wafanyabiashara wadogo
ZANZIBAR; Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ametekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020 kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuwatengenezea mazingira mazuri rasmi ya kuyafanyia biashara zao ikiwemo mama ntilie, mafundi gereji, wafua vyuma, wauza mbao na wengineo.
Dk.Mwinyi amesema hayo leo tarehe 25 Oktoba 2023 wakati akifungua kituo maalum cha wafanyabiashara na wajasiriamali Kitogani, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Pia Dk.Mwinyi ametoa wito kwa halmashauri kuweka viwango vya kodi kwa wajasiriamali vinavyohimilika na siyo kuweka kodi za bei ya juu.
Vilevile ameagiza wafanyabiashara na wajasiriamali watakaoanza kufanya biashara kituo hicho wasilipe kodi kwa miezi mitatu.