Serikali yasitisha kilimo kando ya Mto Ruvu

PWANI: MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesitisha kwa muda shughuli za kilimo kando ya Mto Ruvu hadi mvua zitakapoanza.
Hatua hiyo imetokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha kupungua kwa kiwango cha maji kwenye mto huo. Kunenge alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua na kutembelea mitambo ya uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Ruvu Juu.
Alisema kuwa wakulima wanaotumia maji ya Mto Ruvu kwa shughuli za kilimo wasitishe matumizi hayo kwa muda, hadi mvua zitakapoanza kunyesha kwa wingi. “Mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kupungua kwa kiwango cha maji hususan katika eneo la Ruvu Chini, hali inayochochewa na ongezeko la shughuli za kibinadamu kandokando ya mto huo,” alisema Kunenge.
Alisema watumiaji wa maji ni wengi na wengine wana vibali, hivyo anawasihi wawe wavumilivu katika kipindi hichi mpaka mvua zitakapoanza kunyesha.
“Uzalishaji wa maji katika mitambo ya Ruvu Chini umepungua, japokuwa si kwa kiwango kikubwa huku Ruvu Juu ikiendelea kuwa na kiwango cha maji cha kuridhisha. Hivyo, wananchi watumie maji kwa umakini na kuyabana kwa matumizi muhimu hadi msimu wa mvua utakapoanza,” alisema Kunenge.
Katika hatua nyingine, aliwashukuru wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwa kutunza vyanzo vya maji vya Mto Ruvu na kuhimiza wakazi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kulipa ankara za maji kwa wakati ili serikali iweze kupata mapato ya kuboresha huduma za maji.
“Kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upungufu wa maji, kwani bwawa hilo litaruhusu uhifadhi wa maji ya kutosha bila kutegemea mvua za msimu,” alisema Kunenge.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na: Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri; Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Pili Mnyema; Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani.




Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com