Serikali yatambua mchango wa BAKWATA

DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatambua mchango wa madhehebu ya dini na wadau wa elimu katika kuimarisha maadili, kuendeleza maarifa na kuleta mshikamano wa kitaifa.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais Dk. Samia katika hafla ya utoaji tuzo za elimu za Mufti zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel. Majaliwa amesema Serikali inathamini juhudi za taasisi za dini kama BAKWATA katika malezi ya watoto na vijana. “Rais Dk. Samia anawapongeza sana BAKWATA kwa juhudi mnazozifanya katika malezi, elimu na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kupitia maadili na maarifa,” amesema.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa tuzo hizo ni jukwaa la kitaifa la kutambua michango ya kipekee katika elimu, ubunifu, malezi na maadili ya vijana wa Kitanzania. “Serikali ya Awamu ya Sita inahakikisha elimu inakuza maarifa na ujuzi sambamba na malezi yanayoimarisha tabia bora na maadili ya kizalendo kwa vijana wa Kitanzania,” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake, Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi, amesemaBAKWATA  imewekeza muda mrefu katika elimu kwa kuanzisha shule, vyuo na madrasa vilivyozalisha viongozi na wataalamu mbalimbali nchini. “Wengi walipitia shule za BAKWATA na leo ni mawaziri, wanasheria, wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa umma. Huo ndio uthibitisho wa mchango wetu katika elimu ya Taifa,” alisema Mufti. SOMA: Bakwata: Tambueni thamani ya kura zenu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button