SGR yasafirisha wajumbe 922 vikao CCM

DAR ES SALAAM; MKURUGEN ZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema wa metoa treni maalumu ya kisasa (SGR) jana kusa firisha takribani watu 922 wanaotarajiwa kushiriki kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unao fanyika kesho na kesho kutwa jijini Dodoma.

Hivyo amewashukuru watu hao wakiwamo wajumbe 600 wa CCM kutumia SGR kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma unapofanyika mkutano huo.

Wajumbe wa CCM kutoka maeneo mbalimbali nchini wanakutana Dodoma kwa Mkutano Mkuu Maalu mu.

Advertisement

Kabla ya mkutano huo, leo kunatarajiwa kufanyika kikao cha Kamati Kuu na kufuatiwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari katikaStesheni ya Magufuli Dar es Salaam jana, Kadogosa alisema, “Wajumbe wa CCM wako zaidi ya 600, kutoka Lindi, Mtwara, Zanzibar yote, Dar es Salaam, Pwani tutawachukua Soga, Morogoro…

lakini pia kuna wageni na wasanii mbalim bali walioalikwa kwenye mkutano huo, tunasafiri sha takribani abiria 922, nawashukuru CCM kwani wangeweza kusafiri kwa kutumia mabasi au ndege, lakini wameamua kutumia treni

“Hii ni biashara tunafan ya lakini sio jambo geni kwa TRC tulishawahi kusafirisha wajumbe kutoka Mwanza,” alieleza Kadogosa.

Alisema usafiri wa SGR ni moja ya mambo yaliyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 – 2025, hivyo wajumbe hao wa CCM ku tumia usafiri huo inawafan ya kujivunia chama chao

“Lazima wajivunie kwamba mambo yali yokuwa wameyaweka kwenye makaratasi sasa yamekuwa uhalisia, unajua chama lazima kiuzwe na kinauzwa kwa mafanikio ya waliyoahidi wananchi kwa miaka mitano… mpango wa SGR upo kwenye Ilani ya CCM nadhani ukurasa wa 59 kama sikosei, na wakati wowote tunatarajia kusaini mkataba wa ujenzi kutoka Uvinza mpaka Msongati,” alieleza Kadogosa.

“Mpaka sasa tangu tumeanza usafirishaji tume shasafirisha abiria takribani milioni 1.4, ni watu wengi sana, wastani wa watu 7,000 mpaka 10,000 kwa siku lakini haimaanishi changamoto hazipo, zipo na watanzania wajue hivyo,” alieleza.

Kuhusu hujuma ya miundombinu, Kadogosa alisema kwa sasa haijatokea tena lakini haimaanishi walale bali wanazidisha mbinu za kukabiliana nazo.