Sh Bil 2.5 kusaidia wajasiriamali ubunifu

Mradi wa ubunifu wa Fungo umetangaza fursa mbili za wajasiriamali na biashara endelevu, ambapo kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 2.5 zitatolewa kwa lengo la kuibua uwezo wa wajasiriamali na kuchochea ukuaji endelevu katika sekta mbalimbali nchini.

Mradi huo wa ubunifu wa kimkakati umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), Jamhuri ya Finland, na Serikali ya Uingereza (FCDO), na kutekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP
Tanzania).

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Uchumi na Utawala wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Karina Dzialowska amesema dhamira ya EU ni kukuza ukuaji jumuishi na ubunifu kwa watanzania.

“ Mradi huu ulianza kama majaribio miaka minne iliyopita, sasa umekuwa mhimili mkuu wa mfumo wa Tanzania, Funguo limekuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara changa kwa msaada wa kiufundi na ufadhili unaowasaidia kukua na kufikia fursa pana za kifedha.

“Ninatoa wito hususani kwa vijana wanawake wenye ndoto na uthubutu, tunakusudia angalau asilimia 40 ya ruzuku hizi ziende kwa wanawake, lakini hili litatimia tu kama mtawasilisha maombi yenu,” amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Ubalozi wa Finland nchini Tanzania, William Nambiza amesema kupitia GreenCatalyst na ushirikiano wake kupitia mradi wa Kusimamia Uhifadhi wa Misitu, Matumizi Bora ya Ardhi na Kuongeza Thamani ya Mazao ya Misitu (FORLAND) wamejikita katika kuzalisha ajira rafiki kwa utunzaji wa mazingira, kulinda rasilimali, na kukuza ubunifu wa ndani kwenye mnyororo wa thamani wa misitu.

Amesisitiza uungaji mkono wa Finland kwa biashara ndogo, ndogo sana na kusema wanataka kuchochea ukuaji wa biashara bunifu katika mnyororo wa thamani wa misitu, na wqnatoa wito kwa wajasiriamali wengi zaidi kuwasilisha maombi na kuchangamkia fursa hii kupitia mpango wa huo wa #GreenCatalyst.”

Naye Naibu Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, John Rutere ameelezea umuhimu wa fursa hizi akisema ni safari ya kujenga kizazi cha biashara zinazotatua changamoto halisi na kuleta mabadiliko endelevu.

Amepongeza mafanikio ya mradi, ambapo zaidi ya ajira 5,000 zimezalishwa na zaidi ya Sh bilioni 15 za ufadhili wa nyongeza zimekusanywa, kufuatia uwekezaji wa Sh bilioni 5.2 kwenye biashara changa 61.

“Fursa hii inawalenga wajasiriamali wanaobuni bidhaa au huduma kama vile useremala wa kisasa, bidhaa za mianzi, vifungashio rafiki kwa mazingira, mkaa mbadala, kilimo rafiki kwa misitu, utalii wa ikolojia, na huduma za kidijitali za misitu.

“Kipaumbele kinatolewa kwa biashara zilizopo au zinazohusiana na mikoa ya Iringa, Njombe,
Ruvuma, na Lindi, mradi unawapa kipaumbele vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu,” amesema.

Amesema biashara zitakazochaguliwa zitapata ufadhili wa kuanzia Sh milioni 10 mpaka Sh milioni 100, pamoja na usaidizi wa kiufundi, kukuza biashara, upatikanaji wa masoko, zana za kidijitali, na mafunzo ya ubunifu unaozingatia mabadiliko ya tabianchi.

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am now making an extra $19k or more every month from home by doing a very simple and easy job online from home. sxs I have received exactly $20845 last month from this home job. Join now this job and start making extra cash online by following the instructions on the given website………………….. ­­W­­w­­w­­.­­J­­o­­i­­n­­S­­a­­l­­a­­r­­y.­­­C­­­o­­­m­­­

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button