Umeme wa Jua Waongeza Nguvu Gridi ya Taifa

SERIKALI kupitia TANESCO imejizatiti kuwekeza katika vyanzo mseto vya nishati ya umeme ikiwemo mashamba ya umeme wa jua ili kuongeza uhakika wa nishati. Mradi wa mashamba haya umeanza kutekelezwa kwa kushirikiana na wawekezaji katika mikoa ya kanda ya Ziwa, hasa Bukombe na Ushetu.

Kaimu Ofisa Mawasiliano wa TANESCO, Augustino Kasale, amesema serikali ipo kwenye mpango wa kuongeza uwekezaji katika nishati ya umeme, ikiwemo mradi mkubwa wa shamba la umeme jua wilayani Kishapu, Shinyanga, utakaozalisha Megawati 50 na baadaye kupanuliwa hadi 150 MW.

Mhandisi msimamizi wa shamba la Bukombe, Givason Bugale, amesema mradi huu unazalisha Megawati 6.5 na kusambaza 5 MW kwenye gridi ya taifa. Mashamba haya ni mradi wa pili kukamilika baada ya Ushetu, na mradi wa tatu unaendelea kujengwa Ikina.

Bugale amebainisha kuwa uzalishaji mkubwa hutokea wakati wa mchana, lakini mabadiliko ya hali ya hewa, kama siku zenye mawingu, hupunguza kiwango cha umeme kinachozalishwa. Kabla ya shamba la Bukombe kuanza, kiasi kikubwa cha umeme kilipotea kutokana na kutegemea kituo cha Nyakanazi.

Lengo kuu la miradi hii ni kuongeza nishati kwenye gridi ya taifa, huku pia ikisaidia kupunguza mzigo kwenye vituo vya kupokea na kusambaza umeme, na hivyo kuongeza uhai wa mashine hizi. SOMA: Bil 2/- kufikisha umeme wa jua Bukoba, Muleba

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button