Sh Bil 61.5 zatengwa barabara za mikoa

DODOMA; SERIKALI imesema kiasi cha Sh Bil.61.5 kimetengwa kwa ajili ya barabara za mikoa na madaraja katika mikoa yote 26 Tanzania Bara mwaka wa fedha 2024/25.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi zilizongwa ni ukarabati wa kilometa 600 kiwango cha changarawe na kujenga kilometa 60 kiwango cha lami.

“Katika mwaka wa fedha 2024/25, jumla ya Sh milioni 61,585.00 zimetengwa kwa ajili ya barabara za mikoa na madaraja katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

“Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ukarabati wa jumla ya kilometa 600 kwa kiwango cha changarawe, kujenga kilometa 60 kwa kiwango cha lami na ujenzi wa madaraja/ makalavati 70.

“Aidha, kati ya fedha hizi, Sh milioni 726.00 zitatumika kwa ajili ya programu ya mafunzo kwa vitendo (Structured Engineers Apprentinceship Programme – SEAP) kwa wahandisi wahitimu,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button