Sh bilioni 1 kuimarisha huduma ya maji Moro

MOROGORO: SERIKALI Kuu imetoa Sh bilioni 1.3 kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa miundombinu ya maji safi na salama katika kata mbalimbali zenye changamoto za ukosefu wa maji Manispaa ya Morogoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, CPA Sais  Kyejo amesema hayo katika taarifa yake kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro ilipotembelea mradi na vyanzo vya maji maeneo ya  Mambogo, Bwawa la Mindu na Mtambo wa kusafisha maji wa Mafiga.

Kyejo amesema licha ya Serikali Kuu kutoa kiasi hicho cha fedha, mamlaka hiyo nayo imeongeza Sh milioni 484 na kufikia jumla ya fedha Sh bilioni 1.8 kwa ajili uendelezaji usambazaji wa miundombinu ya maji na kulaza mabomba ya maji kilometa 194 maeneo ya  Lukobe, Mkundi na Kiegea ambayo yanakabiriwa na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Amesema katika utekelezaji wa usambazaji wa miundombinu ya maji, wananchi wapatao 1,828 wa maeneo hayo hadi sasa tayari wameshaunganishiwa huduma ya maji safi na salama.

“Awamu ya kwanza  wananchi hawa wameshaunganishiwa maji na sasa tunaendelea na awamu ya pili kwa kulaza mabomba ya maji kilometa 268 na mzabuni amepatikana na mabomba yameanza kuletwa “ amesema CPA Kyejo.

Amesema Mamlaka inaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa usambazaji wa huduma ya maji maeneo ambayo hayajawahi kuwa na miundombinu ikiwemo Kata ya Kingolwila na maeneo jirani.

Ametaja maeneo yanasambaziwa mabomba kwa mara ya kwanza katika kata hiyo ni mtaa wa shule ,Tambukareli, Zahanati, Kitungwa, Korogoso na Bomba la  Zambia na kazi hiyo imefikia hatua nzuri ambapo wananchi wameanza kupata huduma ya maji safi na salama.

“ Hali ya upatikaji wa maji imeimarika kwa vyanzo vya milimani vilivyopata changamoto wakati wa kiangazi na uzalishaji kwenye  Bwawa la Mindu unaendelea zaidi ya lita milioni 30 wastani kwa siku,  hali si mbaya kwa sasa “ amesema  CPA Kyejo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa huo ,Mhandisi Joseph Masunga aliitaka Moruwasa pamoja na Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu kuhakikisha wanadhibiti shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na baadhi ya wananchi kando kando ya vyanzo vya maji.

Ametaka hatua za haraka zichukuliwe kusimamisha shughuli za uchimbaji wa madini na wachimbaji waondolewe ili maji yaendelee kuwa salama na kulinda mazingira kwa ujumla.

Mhandisi Masunga amesema  kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro wanategemea kupata maji safi kutoka katika vyanzo hivyo.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  www.join.work27.com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do………………………………………………………………………………………………………………………………………………………  www.join.work27.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button